Matumizi Mabaya Ya Simu ( Smart Phone ) Ki Afya Na Kijamii.

Matumizi ya simu za mkononi yana hatari nyingi za kijamii na kiafya kwa watoto na vijana walio chini ya umri wa miaka 20.

Inashauriwa kuwa ni bora kwa vijana hawa kuepuka matumizi ya simu za mkononi au watumie mara chache sana tena kwa muda mfupi na pale inapokuwa hakuna njia mbadala ya mawasiliano.

Matumizi makubwa ya simu za mkononi yanaingilia utendaji wa ubongo wa vijana wadogo. Huathiri uwezo wa kufikiri sawasawa na kuwa makini lakini pia inasemekana kuwa, matumizi makubwa ya simu hizi katika umri mdogo, yanaongeza uwezekano wa kupata kansa ya damu kutokana na mionzi.

Vijana wanaotumia simu za mkononi kwa muda mrefu hukabiliwa na msongo, kukosa utulivu wa kiakili, hali ya kupata uchovu wa mwili na hali ya kutokupata usingizi vizuri.

Wengi hawazimi simu zao wanapokwenda kulala usiku na wengine hulala nazo kitandani karibu kabisa na kichwa, jambo ambalo huharibu mtiririko wa usingizi wakati akili inapohitaji kupumzika.

Jumbe na miito mingi ya wasichana huwa inahusiana na mambo ya kimapenzi ambayo huchochea akili kufikiria ngono kwa nguvu kutokana na ukweli kuwa wakati wa balehe, tamaa za ngono huwa na nguvu kubwa.
Simu zenye mtandao pia huwaingiza vijana wengi katika mtego wa kuangalia picha za ngono zinazochochea tamaa ya ngono haramu na hatarishi.
Akili za watoto, ikiwa ni pamoja na wasichana hudhurika kirahisi kwa mionzi na athari zake kuchukua muda mrefu hata baada ya matumizi ya simu kwa muda mfupi.

Mionzi ya simu hupenya katika fuvu la watoto kwa nguvu zaidi kuliko watu wazima waliokomaa.

Uwezo wa kiakili wa vijana ambao unatazamiwa kuwa utapungua wafikapo katika umri wa kustaafu kazi (miaka 60), hupunguzwa na mionzi ya simu. Wafikapo miaka 30 tu ya umri wao, vijana wanao tumia sana simu za mkononi, huwa sawa na wazee wa miaka 60 katika uwezo wa kiakili.
Tafiti kadhaa huonyesha vijana wenye umri wa miaka 20 wakiendesha gari huku wanaonge kwa simu uwezo wao wakiakili wa kufanya maamuzi huchelewa sawa na ule wa wazee wa miaka 70. 
Umakini wao hugawanyika katika kuangalia usalama na kutafakari maana ya ujumbe na jinsi ya kujibu. Mionzi pia huvuruga uwezo wa ubongo wa kufanya maamuzi kwa haraka.

Mara nyingi matokeo ya jambo hili huwa ni ajali za barabarani, zinazo sababisha madhara makubwa ya kiafya na ulemavu au vifo.

Upo ushahidi pia unaoonyesha kuwa kutumia simu kwa muda mrefu husababisha maumivu ya kichwa na hisia ya ganzi katika ngozi ya kichwa.

Mionzi ya simu za mkononi pia hupunguza uzalishwaji wa kichocheo cha melatonin mwilini ambacho ni muhimu kwa utendaji mzuri wa ubongo na kinga dhidi ya saratani ya matiti. 

Wasichana wanaotumia simu za mkononi kwa muda mrefu, wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya matiti na ugonjwa wa ubongo (Alzheimer’s disease) mapema au baadaye sana katika kipindi chote cha maisha yao yaliyobaki.

Hii inatokana na uwezo mkubwa wa seli za vijana kuitikia nguvu za mionzi. Hali huwa mbaya zaidi kama simu inatoa mionzi zaidi ya kipimo cha SAR (Specific Absorption Rate) Wart 2/kg.

Tatizo jingine la kiafya kutokana na simu ni ugonjwa wa masikio kuunguruma muda wote (Tinnitus) hasa kwa wasichana wanaosikiliza muziki kwa kutumia simu zao au kupokea miito ya simu yenye makelele kupitia vipokeleo vya sauti vinavyobandikwa masikioni (ear phone).

Athari nyingine za matumizi ya simu ya mkononi kwa msichana ni athari za kijamii. Wasichana wengi wamekuwa walengwa na wahanga wa ngono hatarishi kutokana na matumizi mabaya ya simu za mkononi.

Wasichana wengi wanaomiliki simu, kutokana na umri wao, wanashindwa kutumia simu hizi kwa ajili ya mawasiliano yenye kuleta faida na matokeo yake huwa ni kujitumbukiza katika hatari nyingi za kimaisha.

Siku hizi simu ya mkononi ndicho chombo kinachotumiwa na wasichana wengi kufanya mawasiliano ya haraka na wale wanaowaita wapenzi wao na kurahisisha mipango ya kukutana na kutimiza matakwa yao.KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA SIMU (SMARTPHONE)
Usipitwe na Habari Yoyote Ya Injiri,Magazeti,mafundisho Ya Biblia,Mahusiano,Afya,Teknolojia Na Exclusive Interview on Togolay24 TV kila siku. Install Togolay24 App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

0 Maoni