UTAMBULISHO KUTOKA PROSPEROUS SOUND KWA MARA YA KWANZA.

Shalom Mtu wa Mungu kwa mara ya kwanza kabisa Kutoka Kwenye Kiwanda cha Burudani ya Muziki wa Injili Nchini Tanzania tunawatambulisha kwako Prosperous Soundsn wakiachia video pamoja na Audio ya Kwanza unaoitwa Hakuna Kama Bwana.Video: Prosperous Sounds - Hakuna Kama Bwana | Download Audio MP3
Prosperous Sounds ni kundi lililowakusanya vijana walioamua kumtumikia Mungu kupitia vipaji vyao uimbaji na wimbo huu ni wimbo wao wa kwanza uliowaunganisha vijana hawa na hakika kupitia ujumbe ulio katika wimbo huu utakiri kuwa umejaa upako, sifa na Ibada kwa ajili ya kuleta uamsho, kuponya, kufariji na kumtia moyo mtu aliyekata tamaa.
Prosperous Sound ni kundi lililozaliwa Disemba 2018 katika mkesha wa vijana siku ya alhamisi ndani ya kanisa la Ufufuo na Uzima Glory of Christ Tanzania Church kwa askofu Josephat Gwajima na kuanzia hapo ndipo kundi lilipoanzishwa ambapo lilianza na watu sita na mpaka sasa lina vijana wasiopungua 42 na kila mmoja akiwa anatumia kipaji alichobarikiwa kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
Mbali na hayo yote moja kati ya viongozi wa kundi hilo Imani Nshoka alisema kuwa wakiwa kama vijana wana maono ya kuuteka ulimwengu huu wa vijana kwa kuhubiri Injili kupitia uimbaji na wana hakika kuwa watafanikiwa kuwarudisha vijana wengi kwa Yesu Kristo maana wana nguvu na uweza unaoongozwa na Roho Mtakatifu.
Tunaamini kuwa utabarikiwa na kuinuliwa kwa namna ya pekee kila wakati utakapokuwa unaitazama video hii iliyobeba habari njema kutoka kwa vijana hawa walioonesha nguvu zao kupitia vipaji vyao kwa ajili ya ufalme wa Mungu, Amen.

KUPATA HABARI ZA KILA SIKU MASAA 24 KWENYE SIMU YAKO KWA KU DOWNLOAD APPLICATION YETU PLAY STORE AU KWA KU BONYEZA HAPA KUI DOWNLOAD <<TOGOLAYA24 APP>>

0 Maoni