Maombi dhidi ya mlipuko wa tauni ya Corona Virus - Mwalimu Mgisa Mtebe

 *Maombi dhidi ya mlipuko wa tauni ya Corona Virus* (na Magonjwa mengine). .KWANZA Tuombe Toba* juu ya uovu na uasi uliofungulia shambulio hili. *2Nyakati 7:12-14*

[12]BWANA akamtokea Sulemani usiku, akamwambia, Nimesikia uliyoyaomba, na mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya dhabihu.
[13]Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, *au nikiwapelekea watu wangu tauni;*

[14]ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na *kuiponya nchi yao*.
.
PILI Tuombee ugunduzi wa dawa*; Mungu awape wataalam akili, ufunuo na maarifa ya kugundua dawa. *2Timotheo 2:7*
[7]Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.
.
TATU. Tuamuru mlima huu ung'oke na kutupwa nje ya dunia.*; kwamba Mungu autokomeze ugonjwa huu kabisa ktk watu na wanyama.

*Marko 11:23*

BWANA Yesu anasema; Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia *mlima huu (ugonjwa wa tauni)*, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo *asemayo yametukia, yatakuwa yake.*
.
NNE. Sifa na Shukurani*
Tumtukuze Mungu juu ya uweza na nguvu zake, kwamba anaweza mambo yote. *Yeremia 32:27*

Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; *je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?*

Ndoa za jinsia Moja za Pamba Moto Marekani | Afrika Wagoma KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, EXCLUSIVE INTERVIEW,MICHEZO,MAFUNDISHO,NA MATUKIO YOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA TOGOLAY24  DOWNLOAD HAPA>

0 Maoni