Haji Manara agoma kuomba msamaha Yanga

BAADA ya uongozi wa Yanga kumpa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara muda wa siku 14 za kuomba msamaha na ikiwa atashindwa watampeleka mahakamani, Manara amesema kuwa hawezi kufanya hivyo kamwe.

Simba SC mocks Yanga transformation

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredric Mwakalebela hivi karibuni aliweka wazi kuwa wanampa siku 14, Haji Manara za kuomba msamaha hadharani kwa kuwa alitumia vibaya mtandao wake wa kijamii kuishusha hadhi jezi ya Yanga.

Mwakalebela alienda mbali kwa kusema kuwa kwa kufanya hivyo kulipunguza mauzo ya jezi za Yanga jambo ambalo wanalihitaji kutoka kwa Manara ni kuomba msamaha hadharani.

"Tunampa Manara (Haji) siku 14 za kuomba msamaha kwa ajili ya kutumia jezi ya Yanga kinyume na utaratibu katika mtandao wake wa kijamii kwa kuweka chapisho ambalo limefanya mauzo ya jezi kushuka.

"Ikiwa hatafanya hivyo siku hizo zikikamilika basi tutachukua hatua ya kwenda mahakamani kumfungulia mashtaka,".

Manara amesema:"Mimi kuomba msamaha siwezi kabisa, haiwezekani jambo hilo kutokea kwa sasa kwani nimezoea kesi tena kesi kama hizi acha kabisa,".

Yanga walitoa kauli hiyo Februari 19,hivyo itakapofika Machi 5 zitakuwa zimekamilika siku hizo 14 ambazo Manara amepewa na mabosi wa Jangwani.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, EXCLUSIVE INTERVIEW,MICHEZO,MAFUNDISHO,NA MATUKIO YOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA TOGOLAY24  DOWNLOAD HAPA>

0 Maoni