Ndege
za kivita za Urusi zimefanya mashambulizi kadhaa ya anga katika maeno
ya wanamgambo wa IS kwenye jangwa la Syria, wanaharakati wamesema
Jeti hizo zinaunga mkono operesheni za vikosi vinavyounga mkono serikali ya Syria ili kudhibiti barabara kati ya Homs na Deir al-Zour, kwa mujibu ya waangalizi.
Wanaamgambo wa IS wamefanya uvamizi na mashambulizi hivi karibuni , tukio la karibuni, siku ya Jumatani, wanajeshi tisa na wanamgambo waliuawa.
Waangalizi
wa haki za binadamu nchini Syria wenye makazi yao nchini Uingereza,
ambao wanafuatilia vita nchini Syria kwa kutumia vyanzo vya kimtandao ,
wamesema watu wengine watatu waliuawa siku ya Jumanne baada ya bomu
lililotegwa ardhini na wanamgambo wa IS kulipuka katika jangwa Kusini
mashariki mwa jimbo la Deir al-Zour
Mashambulizi ya anga ya Urusi siku ya Jumanne yaliua wanamgambo takribani 10 mjini Deir al-Zour na katika jimbo la Hama, wakati kukiwa hakuna taarifa za madhara kutokana na mashambulizi ya Jumatano katika eneo la al-Shawla.

Televisheni ya Syria, Televisheni ya upinzani, pia imesema kuwa ndege za Urusi zilikuwa zikishambulia maeneo ya wanamgambo wa IS kwenye jangwa mkoa wa Badiya.
Hatahivyo, vyombo vya habari vya serikali havisema chochote kuhusu operesheni iliyoripotiwa.
Katika
tukio tofauti siku ya Jumatano, polisi wa Uturuki walisema wamewakamata
wanachama wawili waandamizi wa IS huko Ankara na kumwachilia msichana
wa miaka saba kutoka jamii ya wachache ya Yazidi ya Iraq ambaye alikuwa
anashikiliwa mateka. Mmoja wa washukiwa alitambuliwa kama afisa wa
zamani wa jeshi la Iraq
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, EXCLUSIVE INTERVIEW,MICHEZO,MAFUNDISHO,NA MATUKIO YOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA TOGOLAY24 < DOWNLOAD HAPA>
0 Maoni