Polepole: Magufuli hana mpango wa kuongeza muhula mwingine

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole amesema kuwa Rais wa Tanzania John Magufuli hana mpango wa kuongeza muda wa kukaa madarakani.

Image result for magufuli

Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji kupitia chama cha ACT-Wazalendo bungeni leo aliibua suala hilo akikosoa wabunge wawili wa CCM ambao walitoa hoja ya kutaka Rais Magufuli kuongezewa muda na Polepole kujibu hoja zao.

Akitoa taarifa kwa mbunge huyo wa ACT, Polepole amesema kuwa Rais hataongeza muda wowote.

“Masuala ya Chama cha mapinduzi hujadiliwa kwenye vikao vya chama , hapa bungeni wabunge wana uhuru wa kuzungumza lakini kinachozungumzwa humu ndani hakiathiri msimamo wa Chama cha Mapinduzi ambao tumeshautoa, Rais hataongeza muda,” ameeleza Polepole.

Mjadala wa kuongeza muda wa rais madarakani umerejea tena hivi karibuni baada ya wabunge wawili wa CCM kuchangia Bungeni.

Awali, katika muhula wake wa kwanza, Rais Magufuli alipuuzia mapendekezo hayo kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Bunge lililopita akiahidi kutoongeza hata dakika moja muda wake wa kuondoka madarakani utakapofika.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, EXCLUSIVE INTERVIEW,MICHEZO,MAFUNDISHO,NA MATUKIO YOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA TOGOLAY24  DOWNLOAD HAPA> 

0 Maoni