UTAJUAJE ANAYE-KUCHUMBIA NI MTU SAHIHI? FANYA HAYA YAFUATAYO - Pastor : Zakayo Nzogere

YAFUATAYO NI MASWALI MATATU MUHIMU AMBAYO MAJIBU YAKE YATAKUPA PICHA YA KUKUSAIDA KUJUA KAMA JAMAA NI MUOAJI AU MBABAISHAJI:
MUULIZE...

1. UNATAKA KUOA LINI??

Hili ni swali muhimu sana kwasababu siyo BUSARA kukaa kwenye mahusiano yasiyo na mipango wala muelekeo. (Undated plan is NOT a plan).

Jibu lake litakusaidia kujua huyo ni mtu mwenye MIPANGO au la. Pia litakuwezesha kuamua kama upo tayari kukaa kwenye uchumba kwa muda kiasi gani endapo mtakubaliana.

⚠️ Kama jamaa hana JIBU au HAJUI hata anataka kuoa lini; basi elewa kwamba jamaa HAJAJIPANGA bado; huyo anaweza kukupotezea muda... ni pasua kichwa🤭🤭

2. KWANINI UNATAKA KUNIOA MIMI??

Hili ni swali kubwa, gumu, lakini pia la muhimu sana. Jibu lake litakusaidia kujua endapo mwanaume huyo anakupenda wewe au kavutwa na kitu tofauti.

Kwa mfano; mwanaume anaweza kuja kwako kwa sababu ya hadhi ya wazazi au familia yenu (status), kazi yako, mali, kipawa chako, au vitu vinginevyo.

📌Endapo majibu yake yataelekea kwenye tabia yako(character), haiba yako (personality), na msimamo wako wa kiimani (spirituality), hayo ni majibu yanayolenga UTU wako... Yani wewe kama wewe!!

⚠️ Lakini ikiwa majibu yake yataelekea zaidi kwenye vitu, nafasi, hadhi, na maslahi fulani; ujue wewe siyo kipaumbele kwake, na pia inawezekana jamaa anatafuta AHUENI ya maisha tu!

3. MIMI NIKISEMA HAPANA, UNADHANI NANI MWINGINE ATAFAA KUWA MKE WAKO??

Hili ni swali la UDADISI la kukusaidia kujua nafasi na umuhimu wako kwenye moyo wake.

⚠️ Akianza kusema, “nadhani Mary, Rose, Betty, au Dada fulani anaweza kunifaa... “; basi ujue kwamba upo katika mchakato wa kushindanishwa na wengine wengi. Yani bado hajaamua anataka nini.

✨ZINGATIA HILI...

📌 MBALI NA HAYO MASWALI MATATU, KIPIMO KIKUBWA KULIKO VYOTE NI ENDAPO HUYO MWANAUME HATA HARIBU MAHUSIANO YAKO NA MUNGU WAKO.

⛔️ Mungu hawezi kukupa mtu atakayekutoa katika uwepo wake!! Kama anakutoa kwa MUNGU, ujue huyo hajatoka kwa MUNGU.

⚠️ TUMIA HEKIMA KUULIZA HAYO MASWALI MATATU; ISIWE KANA KWAMBA MTU YUPO KITUO CHA POLISI🤣🤣. ULIZA KIRAFIKI LAKINI KWA KUMAANISHA. SI LAZIMA KUULIZA YOTE

Faida ya Upendo na Kusamehe - Pastor John SembatwaKWA HABARI, LIVE TV, RADIO, EXCLUSIVE INTERVIEW,MICHEZO,MAFUNDISHO,NA MATUKIO YOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA TOGOLAY24  DOWNLOAD HAP

0 Maoni